Inajulikana kwamba mbwa ni rafiki mkubwa wa binadamu ambapo licha ya kuumbwa kuishi karibu na binadamu, wanayama hawa wanatajwa kuwa miongoni mwa viumbe wenye akili ukimuondoa binadamu. Wako vizuri kwenye kuwinda, ulinzi na wakati mwingine hutumika kama mwandani katika matembezi ya binadamu.
Hata hivyo, kuna report zinazoonesha kuwa Mbwa wanaweza kuwa maadui wakubwa wa binadamu na zipo aina nyingi za Mbwa lakini zipo zinazotajwa kuwa tishio zaidi duniani.
10 Dobernman Pinschers
Mbwa huyu anajulikana kuwa na akili na mwenye nguvu nyingi. Anafaa sana kuwa mlinzi mzuri kwa binadamu. Pia huwa wanatumiwa na Polisi kutafuta wahalifu lakini hata hivyo asipopata mafunzo mazuri anaweza kuwa tishio na anaweza kumuua binadamu.
9 Huskies
Mbwa huyo ni maarufu sana kutokana na macho yake ambayo ni tofauti na mbwa wengine. Wanatumika sana kwenye michezo ya kuteleza kwenye theluji na wanajulikana kuwa na uwezo mkubwa wa kusukuma vitu kwa muda mrefu kuliko mbwa yeyote.
8 Bullmastiff
Mbwa huyu anajulikana kuwa mkali na hatari Sana. inashauriwa kuweka watoto mbali naye. Zipo kuwa mwaka 2014 mbwa aina hii aliwashambulia vijana wawili waliokuwa wakicheza mpira kwenye nyumba ya jirani. Kijana mmoja aliuawa na baada alimshambulia mmiliki wake. Wanatumika sana kwenye ulinzi na wana maumbo makubwa.
7 Wolfdog
Huyu ni mchanganyiko wa uzao wa Ujerumani na Shepherd ambapo mchanganyiko huu unafanya mbwa huyu kuwa mkali sana. Wanaweza kubadilika kutona na hali watakayokutana nayo.
6 Midacet Sula Shephard
Mbwa huyu anatoka kwenye uzao usiojulikana, dhumuni la mchanyiko huo ni kupata mbwa mkali na hatari zaidi Duniani. Mbwa huyu angefaa kulinda binadamu lakini kutokana na ukali wake hawezi kuwa karibu na binadamu na amezuiliwa kwenye baadi ya nchi.
5 Fila Brasileiro
Kama hupendi Mbwa mkali basi usimiliki mbwa huyu. Asili yake ni Brazil na hutumika kwenye shughuli za uwindaji. Anatajwa kuwa mkali na hatari kwa binadamu.
4 Rottweller
Kama kuna mbwa aliyesababisha vifo vingi ni huyu. Imeripotiwa kuwa Mbwa huyu amesababisha vifo vingi Marekani. Wana uwezo wa kuruka juu sana na kudhuru koo la binadamu. Inashauriwa kuwa mbali na mbwa huyu.
3 Perro de Presa Canario
Mbwa huyu ametoka kwenye Visiwa vya Canary. Alitengezwa kwa kutumia mchanganyiko wa mbwa tofauti ili apatikane mbwa mwenye uwezo wa kupambana na wahalifu.
2 Pitbull
Mbwa huyu amezuiliwa kwenye nchi nyingi duniani kutokana na ukali wake na ni hatari kwa binadamu. Aina hii ya mbwa kama hawajafunzwa tangu utotoni wanaweza kuwa mashine ya mauaji. Hutumika kwenye mashindano halifu ya kupigana na mbwa wengine mpaka kifo na wamiliki wao hujipatia pesa kupitia biashara hiyo.
1 Caucasian Shepherd
Asili ya mbwa huyu ni Urusi ambapo kwa karne kadhaa amekuwa akitumika kulinda mashamba ya mifugo milimani. Ana uzito unaokadiriwa kufika zaidi ya KG 100 (220lb) ambao ni uzito wa misuli pekee.
Post a Comment