Kuna njia nyingi ambazo wakulima wanaweza kupata pesa kutokana na ufugaji wa ng’ombe wa maziwa.
Unaweza kutengeneza pesa kutokana na kuuza samadi, ndama wako, na muhimu kabisa uzalizaji wa maziwa mengi.
Kuwekeza kwenye ng’ombe wa maziwa kwanza unahitaji kuorodhesha gharama zote utakazokumbana nazo. Hizi ni pamoja na :
- Banda la ng’ombe
- Vifaa vya kukama maziwa
- Lishe: Unaweza kupanda malisho kama Calliandra na Napier kwenye shamba lako.
- Madini ya kuongeza
- Daktari wa mifugo na ada za madawa.
Malisho
Kutengeneza maziwa mengi mazuri, ng’ombe wa maziwa wanahitaji lishe bora ya aina tofauti, ikiambatana na nguvu, mchanganyiko wa kiwango, protini, vitamin na madini.
Nguvu
Unapolisha ng’ombe wako, mpe mchanganyiko wa chakula kikavu nusu na malisho mabichi nusu.
Malisho mabichi
Malisho mabichi hususani huwa nia mjani kama vile nyasi za Napier, Lucerne na majani ya viazi vitamu na mengineyo. Hivi huwa vina maji mengi.
Usilishe nyasi zilizotoka tu kukatwa kwa ng’ombe wako. Kata majani mabichi na uyaache sehemu yenye giza kufifia, kisha kata kata vipande vya inchi 2 ( 5cm) ili kumrahisishia ng’ombe wako kula. Hii haitapoteza malisho.
Ng’ombe wa maziwa anatakiwa kupewa kilo 15-20 za majani mabichi kwa siku, inapendekezwa kwa awamu mbili kwa mfano.moja asubuhi na nyingine jioni.
Malisho makavu
Malisho yanajumuisha vitu kama Mabua ya ngani, Mabua ya mpunga, Mabua ya mahindi na mazao mengine ya mboga mboga
upande wa mabua na pia kiwango kibaya.
Changanya sehemu moja ya malisho mabichi na sehemu moja ya malisho makavu kwa mfano gunia 1 la nyazi za Napier zilizokatwa katwa na gunia 1 la mabua ya ngano yaliyokatwa katwa.
Protini na chakula cha ziada
Dania
Dania ni chanzo kizuri cha protini. Ng’ombe wako wanatumia protini kwaajili ya kujenga mwili na kuzalisha maziwa mengi ya kiwango bora.
Kilo 5 za Dania kwa siku ni protini ya kutosha kwa ng’ombe wako. Kama ng’ombe wako hawezi kupata protini ya kutosha kutoka kwenye malisho, tumia chakula cha ziada kama Kupakulakutoka Cooper-K Brands.
Chakula cha ng’ombe wa maziwa
Chakula cha ng’ombe wa maziwa kitampa ng’ombe vitamin, nguvu na protini katika njia ya uwiano, ili ng’ombe aweze kuzalisha maziwa mazuri na kuwa na uzito wa mwili wenye afya. Unga Farm Care (EA) wanapendekeza kulisha ng’ombe wako kilo 1 ya Fugo Dairy Meal kwa kila lita 2 za maziwa ng’ombe anazokupatia zaidi ya lita 5 za kwanza.
Hivyo, kama ng’ombe wako anakupa lita 7 kwa siku: 7-5 =kilo 1 ya dairy meal.
KupaKula
Kwa ng’ombe wanaotoa lita 5 – 10 za maziwa kwa siku, wape gramu 400 za Kupakula. Mpe nusu asubuhi na nusu jioni. Kwa ng’ombe wanaotoa zaidi ya lita 10, ongeza gramu 400 kwa siku kila kwa lita 5 zaidi za maziwa juu ya lita 10. Hivyo kwaajili ya lita 20 , mpe kilo 1.2 kwa siku.
Vitamini na Madini
Kumpa ng’ombe wako madini kutafanya biashara yako ya ng’ombe wa maziwa kuwa nzuri. Ng’ombe wako atapata joto siku 60 baada ya kupata ndama hivyo utapata ndama ndani ya mwaka. Madini pia ni mazuri kwaajili ya uzalishaji wa maziwa na hali ya mwili. Madini ya poda, kama Maclik Plus na Maclik Superkutoka Cooper- K Brands ni mazuri kwaajili ya ng’ombe wakubwa. Changanya madini na chakula.
Maclik Plus
Kwaajili ya mtamba na ng’ombe aliekausha mwenye mimbaMpe gramu 10 ( ½ glasi) ya Maclik Plus kila siku.
Maclik Super
Kwaajili ya ng’ombe anaekamuliwa
Mpe gramu 200( glasi 1 ) ya Maclik Super kila siku.
Panda malisho mazao yako ya malisho kama Dania na Nyasi za Napier. Tumia samadi kutoka kwa ng’ombe wako kama mbolea.
Maji mengi
Maziwa yanatumia maji mengi. Unahitaji kuwapa ng’ombe wako maji safi mengi kila siku. Toa maji kwenye chombo cha maji kila baada ya siku 3 na weka maji safi. Hii inazuia magonjwa.
Kujenga banda la Ng’ombe
Hii ni sehemu kwaajili ya ng’ombe kupumzika na kulala wakati wa usiku. Kila ng’ombe ana nafasi yake katika eneo la kumpuzikia, linaitwa . Vyuma lazima vifunikwe na paa lilotengezwa kwa mabati, nyasi au makuti.
Paa lazima liwe juu vya kutosha ili lisiliwe na ng’ombe kama limetengenezwa kwa nyasi au hay inahifadhiwa chini yake.
Vyumba lazima vijengwe kiasi kwamba ng’ombe anabakia msafi muda wote.
Safisha banda la ng’ombe kila siku.
Sakafu ya zege itamzuia ng’ombe asiteleze. Sakafu yenye mwinuko itasaidia uchafu kutoka na ujikusanye nje ya banda.
Safisha na weka viuatilifu kwenye sakafu kila siku. Hii inazuia kuoza kwa kwako na nyayo.
Ng’ombe anahitaji nafasi ya kulala. Mtu anapaswa kujenga idadi ya kutosha ya vyumba ili kutosheleza ng’ombe muda wote. Vyumba visivyotumika ni uharibifu wa nafasi na pesa.
Kwa idadi ya ng’ombe kwa kila vyumba, vyumba vya ziada vinahitajika kuweza kuweka ndama wadogo ( mitamba) na kadhalika.
- Ng’ombe 1 vyumba 2
- Ng’ombe 2 vyumba 3
- Ng’ombe 3 vyumba 5
- Ngombe 4 vyumba 6
- Ng’ombe 5 vyumba 7
- Ng’ombe 6 vyumba 9
Chumba kina urefu wa 210cm ( futi 7) na upana wa 120 cm ( futi 4). Vyumba vinatenganishwa na mbao 2. Ng’ombe hawatakiwi kuzunguka ndani ya chumba.
Chakula ndani ya sehemu ya kulia angalau futi 3 juu ya ardhi. Weka jiwe la madini katika kila chumba kuzuia kupigana kati ya wanyama.
Magonjwa na Chanjo
Njia nyingine ya kuzuia magonjwa ni kupitia chanjo. Hapa chini kuna orodha ya baadhi ya magonjwa ya kawaida unayopaswa kuchanja katika hatua tofauti. Hakikisha unapata Mtaalamu wa mifugo kuchanja ng’ombe wako. Usifanye mwenyewe.
Brucellosis
Umri: Miezi 3-8 kwaajili ya mitamba.
Upeaji:Mara moja katika maisha.
Maoni: Wakati wa mlipuko kundi lote linaweza kuchanjwa.Tumia chanjo kwa umakini. Chanjo ya S19 inaweza kusababisha brucellosis kwa binadamu.
Anthrax and Blackquarter
Umri: Miaka 3
Upeaji: Kila mwaka au kukiwa na onyo dhidi ya mlipuko
Maoni: Chanjo inapatikana na ni ya ufanisi. Anthax ni hatari sana kwa binadamu na wanyama.
East Coast Fever
Umri: Mwezi 1 na zaidi
Upeaji: Chini ya masikio
Maoni: Wataalamu wa mifugo walio na vibali pekee ambao wamefunzwa kuhusu njia za maambukizi na tiba za kutoa ndio wanapaswa kutumiwa
Ugonjwa wa Kwato na Midomo
Umri: Wiki 2 na zaidi
Upeaji: Kila baada ya miezi 6 katika maeneo hatarishi
Maoni: Njia totauti zinatumika. Wasiliana na mtaalamu wako wa Mifugo kuhusu chagua la chanjo.
Rabies
Umri: Miezi 3 na zaidi
Upeaji: Ng’ombe anaweza kuchanjwa kila mwaka na lazima achanjwe kunapokua na mlipuko
Maoni: Hii ni chanjo pekee ambayo inaweza kukinga ng’ombe ambao wameshaathirika kama itafanywa ndani ya muda usiozidi wiki moja baada ya mlipuko. Toa ripoti ya tatizo haraka kwa mtaalamu wa mifugo katika eneo lako
Rift Valley Fever (RVF)
Umri: Miezi 6 na zaidi
Upeaji: Baadhi ya chanjo ni chanjo hai hivyo tumia kwa uangalifu. RVF kwa binadamu inaweza kuuwa hivyo kinga ni muhimu sana.
Lumpy Skin
Umri: Mwezi 1 na zaidi
Upeaji: Kuzuia kunapokua na mlipuko.
Maoni: Kama unatumia chanjo hai, tenga ng’ombe kutoka kwa kondoo na mbuzi, kwani chanjo hutokana na virusi vya pox vya kondoo vilivyo ambavyo vinaweza kusababisha pox kwenye kondoo na mbuzi.
Thank you for a good livestock education, how much is the price of cattle?
ReplyDeleteElimu nzuri
ReplyDeletePost a Comment