Hawa ni kuku wanaofugwa kwaajili ya nyama. Kuku wa Kenchic kama chaguo, ni walaji wazuri na wanakua haraka sana. Wanakua tayari kwa kuuzwa katika umri wa wiki 4 mpaka 5, wanapokua na uzito wa kilo 1.5 mpaka 3. Kuku wako wataweza kupata upeo wa uzito huu kama utawalisha kwa usahihi.
Kuku wa nyama ni biashara yenye faida na manufaa, hata hivyo, sababu inayofanya wafugaji wengi wa kuku wa nyama kutofanikiwa au kupata hasara, ni kwasababu wanaanza bila mpangilio wa biashara. Hiki ni kitu cha kwanza na moja wapo ya vitu muhimu wanavyohitaji kupanga.
Mpango mzuri wa biashara utaonyesha malengo unayotarajia kufanikisha na jinsi unavyopanga kufikia huko. Pamoja na hayo itakuruhusu kujua soko lako kabla ya kuanza ufugaji halisi wa kuku wa nyama. Unaweza kufanya mipango ya uuzaji kwenye hoteli mitaani, mashule, migahawa,mkahawa,madukani na watumiaji wengine wa mara kwa mara.
Kama utajua soko lako kabla ya kuanza biashara yako utakua na uhakika wa kuuza kuku wako wa nyama mara tu wanapokomaa na kuwa na biashara yenye mafanikio.
Lazima pia uweke kumbukumbu nzuri za ufugaji na mahesabu ya uendeshaji wa biashara yako. Hii itakufanya ufatilie kama unatengeneza faida au la.
Kujenga banda la kuku
Banda zuri la kuku litawaweka kuku wako salama na wenye afya. Safisha kila siku. Funga banda kuzuia watu na wanyama kuingia ndani. Wanaweza kueneza magonjwa.
- Jenga banda lako kutoka Mashariki kwenda Magharibi. Hii inazuia jua kali na upepo mkali.
- Kuta za urefu wa futi 4 kwenda juu na futi 3 wavu. Wavu unaruhusu uingiaji mzuri wa hewa.
- Weka mapazia kwenye madirisha kuzuia upepo. Yafunge wakati wa usiku.
- Mahali pa kuoshea miguu na viuatilifu kutazuia wadudu na magongwa. Daima vaa koti na safisha mikono wakati unahudumia kuku.
- Tengeneza sakafu tambarare ya saruji. Sakafu za saruji ni rahisi kusafisha. Maranda ya mbao kwenye sakafu yatanyonya kinyesi yanayodondoka.
- Kila kuku wa nyama anahitaji angalau nafasi ya futi 1 ya mraba. Hakikisha unajua kuku wangapi unapanga kufuga kabla ya kujenga banda.
Kujenga Kiota
Nunua vifaranga vya siku moja kutoka Kenchic. Tayarisha kiota kiwe tayari masaa 24 kabla ya vifaranga vyako kufika. Kiota kiwe na mwanga wa kuyosha. Kiota cha duara kitazuia vifaranga wasibanwe kwenye kona. Panua kadri vifaranga vyako vinakua.
- Unahitaji treya 5 za kulishia na vinyueo 10 vya maji kwa kuku 500.
- Tibu vyombo vyotte kabla ya kuvitumia.
- Kuku yoyote asitembee zaidi ya mita 1.5 kutafuta chakula ama maji.
- Weka jiko futi 1 juu katikati ya banda. Litawapa joto vifaranga kuanzia siku ya kwanza hadi 14 – 21 za mwanzo. Washa jiko masaa 6 kabla ya vifaranga kufika.
Ulishaji wa kuku wako
- Siku 1-21: Starter Mash. Kila kifaranga atakula kilo 1 ndani ya siku 21.
- Siku 21 – 35: Finisher Mash. Kila kuku atakula kilo 2 ndani ya siku 14.
- Siku 35 – 42: Finisher Mash. Kila kuku atakula kilo 1 zaidi ndani ya siku 7.
Badilisha chakula taratibu:
- Siku 20: 75% Starter Mash na 25% Finisher Mash
- Siku 21: 50% Starter Mash na 50% Finisher Mash
- Siku 22: 25% Starter Mash na 75% Finisher Mash
Wakati kuku wako nje ya kiota, toa treya za kulishia. Ning’iniza vilishio kutoka kwenye dari kimo au urefu wa mogongo wa kuku. Hii huzuia kuku kuharibu chakula.
Kuku wa nyama yako itakuwa tayari kwa ajili ya kuuza kwa siku ya 35-42 katika 1.5kg.Magonjwa ya kuku
Ni kawaida hadi asilimia 1 ya vifaranga wako kufa ndani ya wiki ya kwanza. Zaidi ya hiyo, unaweza kuwa na tatizo, kama ugonjwa. Magonjwa kama Ugonjwa wa kideri ama sotoka na Gumboro hayana tiba. Kuku wako wote wanaweza kufa kwa haraka sana. Chanja kuku wako kuzuia magonjwa.
Dalili za Ugonjwa wa Sokota sokota(Newcastle Disease/NCD)
Chanja kwa ajili ya NCD(Kideri) siku ya 7 na 21. Weka tone moja la chanjo kwenye jicho la kuku au tundu ya pua. Ngoja kuku apepese au avute pumzi ndani. Nunua chanjo kutoka kwa wauza pembejeo. Chanjo inaitwa Avivax Kenya na Temevac Tanzania. Chupa 1 inachanja kuku 50. Chanja kila miezi 3.
Dalili za Gumboro
Peleka aliekufa kuku kwa dakitari wa mifugo achune ngozi. Kama kuna alama za damu, kuku wako amekufa kutokana na Gumboro.
Chanja Gumboro siku ya 10 na siku ya 14.
Changanya chanjo pamoja na maji ya kunywa ya kuku. Usiwape kuku maji kwa saa 1 – hadi 2 kabla ya chanjo. Watakua na kiu na hivyo watakunywa chanjo.
Bless san
ReplyDeleteGood I have learned a lot
ReplyDeleteI NEED YOUR CONTACT FOR LEARNING AND ASK MORE QUESTION
ReplyDelete0764905449
DeleteArusha mna mawakala?
ReplyDeleteNahitaji mayai ya kuku wa nyama
ReplyDeleteVipi kuhusu sasso
ReplyDeleteMimi ni mfugaji wa kuku wa nyama lakini kunaungonjwa umetokea kuku mpka nakina la kufuga . Kuku kufuga kwrnye koi anapopumua na Montoya yamemushuka kichwa chaangalia juu
ReplyDeleteKuku anapohema anafura kwenye koo na manyoya yamemushuka na kichwa chaangalia hii mpka anashindwa kula nisaidieni tafadhali
DeletePost a Comment