UKITAKA KUANZISHA MRADI WA KUKU ZINGATIA HAYA;


UKITAKA KUANZISHA MRADI WA KUKU ZINGATIA HAYA;

1. Malengo yako, je unahitaji wakue uwauze tu? unahitaji kupata mayai na vifaranga kwa biashara? Iko hivi, kuku mzuri sana kwa nyma sio mzuri sana katika utagaji na huo ni ukweli usiopingiga. Ukiona mtu anakuambia anavyote at best level achana naye anakudanganya, Na si kwamba akiwa na nyama hatagi no, sema utagaji wake sio mzuri kama wa wale wadogo wadogo na kinyume chake.
2. Uwezo wako, nayo ni point ya msingi kwani usijeukafuga wengi usioweza kuwatunza, nakushauri umpate mtaalam akuandalie bajet ili ujipime kulingana na uwezo wako, ukikurupuka mara nyingi utaishia kujilaum.
3. Usimamizi wa mradi, lazma ujue huo mradi atausimamia nani, wewe mwenyewe au mtu mwingine kwa niaba yajo. Inabidi ufanye maandalizi ili uweke mpangilio utakaokupa wasaa mzuri wa kutekeleza majukum yako kama utasimamia mwenyewe, ikiwa ni pamoja na kutafuta utaalam kwanza kabla hujaingiza vifaranga. Kama utamtumia mtu lazma naye umtafutie utaalam ili awe na walau basic knowledge kwa ajili ya kulea mradi. ukibeba beba tu mtu na kumpa afanye unaweza kulia ndani ya wiki wakafa wote.
4. Mazingira utakayofugia, hapa zingatia usalama wa kuibiwa, wadudu, wanyama, magonjwa ya kuenezwa, muingiliano nk.
5. Soko linataka nini, fuga kitu kitakupa uhakika wa biashara lakini epuka kabisa biashara za msimu/ biashara za kuzuka. Ukijiingiza kwenye biashara hizo mara nyingi huwa zinakuwa na ukomo/ kuisha fasheni. ukiingia kwenye kufuga kwa fasheni maana yake unaweza ingiza gharama zako na saa ya kuvuna ukajikuta soko la bidha zako lishaisha au kuwa dogo..

Post a Comment

Previous Post Next Post