Kuku wa kienyeji wanatofautiana kwa umbo na rangi lakini wote wanafanana kwa mambo yafuatayo. Kwanza woteni wadogo kwa umbo na wana wastani wa uzito wa kilo 1 hadi kilo 2 wanapofika umri kamili. Kutaga kwao huwa kwa kipindi, na kwa wastani hutaga mara tatu kwa mwaka. Wataalam wachunguzi walifanya majaribio na wakaona kuwa kuku wa kienyeji alitaga wastani wa mayai 72 kwa mwaka ambapo kuu wa kigeni alitoa wastani wa mayai 182 na zaidi kwa mwaka.
Kuku wa kienyeji hutaga mayai madogo yenye uzito wa gram 28 hadi 42, ambapo kuku wa kigeni hutaga mayai makubwa kati ya gramu 56 hadi 70. Kuku wa kienyeji huanza kutaga wakati amefikia kwenye umri wa majuma 20. Kuku hawa wa kienyeji huchelewa kukua. Wanafikia uzito wa kilo moaja na robo wakati wana umri wa majuma 21, ambapo baadhi ya kuku wa kigeni wanaweza kufikia uzito wa kilo moja na nusu kati ya majuma 8 hadi 12.
Lakini kuku wa kienyeji wanazo tabia ambazo ni nzuri na zenye faida katika ufugaji.
◾Kwanza ni hodari kujitafutia chakula chao wenyewe.
◾Pili wanao uwezo wa kulalia mayai na kuangua vifaranga, ambapo kuku wa kigeni wamepoteza uwezo huu.
◾Tatu kuku wa kienyeji wanahimili sana harubu za magonjwa mengi ya nchi hizi za joto.
◾Mara nyingi ni majasiri kwa kujilinda kutokana na wanyama kama vicheche na ndege kama mwewe, ambao huwashambulia mara wanapowaona.
Kuku wa Kigeni
Light Sussex
Tanzania ina aina nyingi za kuku wa kigeni nao wamegawanyika katika mafungu makubwa matatu.
Kuku wa mayai
Kuku hawa ni wadogo kwa umbile na hutaga wastani wa mayai 230 kwa mwaka. Kuku wa mayai wamepoteza uwezo wao wa kulalia mayai na kuangua vifaranga. Kwa sababu hii wanapoanza kutaga huendelea kwa muda wa mwaka na zaidi iwapo watapewa mazingira yanayohitajiwa. Kuku mashuhuri na anayefahamika sana katika kundi hili ni Yule kuku mweupe anayefahamika kwa jina la White Leghorn.
Kuku wa nyama
Kuku hawa hufugwa kwa madhumuni ya kupata nyama tu. Kuku hawa wanaweza kutaga mayai iwapo watawekwa mpaka wafike wakati wa kutaga, lakini hutoa wastani wa mayai 170 kwa mwaka, ambayo hayatamletea faida mfugaji akilinganisha na gharama za matunzo ya kuku huyo kufikia muda wa kutaga. Tanzania wapo kuku aina Anak, Cobb na Chunky
Post a Comment