Ugonjwa huu hushambulia wanyama kama ng'ombe, mbuzi na kondoo na husababishwa na vimelea vijulikanavyo kama Theileria parva ambavyo vusambazwa na kupe wekundu wa kwenye masikio wajulikanavyo kama Rhepicephalus Appendiculatus, ugonjwa huu usipodhibitiwa unaweza kusababisha vifo vya wanyama wengi sana na pia ni aghali kuutibu kulinganisha na magonjwa mengine
DALILI
Homa kali,
mnyama kushindwa kupumua vizuri,
kukohoa pamoja na kutoa makamasi,
kuharisha na kuvimba matezi
MATIBABU
Mnyama inabidi apigwe sindano ya dawa za PARVAQUONE au BUTALEXkiasi cha ml 20 (soma kimbatanisho cha dawa kwa maelezo zaidi) na kurudia baada ya siku moja kupita, yaani ukuchoma leo unarudia dozi kesho kutwa, pia mnyama achomwe dawa yaOTC20% kipindi chote cha matibabu
KINGA
Kinga kubwa ya ugonjwa huu ni kuhakikisha kwamba mifugo yako inaoga mara kwa mara kwenye majosho au kwa kuwanyunyuzia dawa za kuua wadudu wa mifugo
NG'OMBE WAKIOGESHWA KWENYE DAWA
Post a Comment