NJIA ASILIA ZA KUTIBU KUKU

njia za asilia za kutibu kuku kwa kutumia shubiri mwitu na majani ya mpapai.

SHUBIRI MWITU NA JINSI YA KUIANDAA

Tafuta majani kadhaa ya shubiri mwitu kisha chana chana vipande vidogo vidogo kisha changanya na pumba na kuvianika.Mchanganyiko huo uanikwe juani.Baada ya kukauka vizuri twanga mchanganyiko huo ma kisha chekecha kupata unga.
majani ya shubiri mwitu
matumizi.
kuku walipata vidonda kutokana na magonjwa mbali mbali ,safisha vidonda vya kuku vizuri kisha pakaa unga huo katika vidonda hivyo.
pia hutumika kama chanjo.
kata kata vipande vidogo vidogo vya majani ya shubiri mwitu kisha changanya na maji na kuku wapewe maji hayo kwa wiki angalau mara tatu.maji yabadilishwe mara kwa mara kabla hayajaharibika.

MPAPAI NA NAMNA YA KUANDAA
mpapai husaidia kuku wanao harisha.
mti wa mpapai
maaandalizi
twanga majani ya mpapai kisha changanya na maji.majani mawili na maji lita mbili au moja na nusu.kuku wapewe maji hayo kwa siku nne lakini maji hayo yatengenezwe kila siku yasiachwe kiporo ili kutumika siku nyingine.
Ikitumika kama chanjo fanya kama ifuatavyo.
andaa kisamvu cha mpapai kisha changanya na pumba kg 2 mwsho weka na maji katika mchanganyiko huo kisha wape kuku lakini chakula hiki kiwekwe kulingana na idadi ya kuku kwa kua kisipo malizika mapema hualibika kirahisi.
kutibu minyoo
unga wa mbegu za mpapai husaidia sana kutibu minyoo katika kuku.

Post a Comment

Previous Post Next Post