JINSI YA KUVITUNZA VIFARANGA.

kitu cha kwanza tambua vifaranga hupendelea kukaa juu, hivyo unatakiwa ujenge banda la ghorofa moja.

Kitu cha PILI tambuwa vifaranga havipendi giza wakati wa mchana, hivyo unatakiwa unapojenga ghorofa yao hakikisha ubavu mmoja una wavu unaopitisha mwanga wa jua. Kitu cha TATU tambuwa vifaranga havitakiwi kuishi pasipo ya mama yao, hivyo hakikisha unapowatenga vifaranga usiwaache pasipo ya mama(hata kama vipo ishirini waweke na mama mmoja tu).

Kitu cha NNE tambuwa vifaranga havitakiwi kupewa maji mengi, hivyo unatakiwa kuwapatia maji machache kwenye vyombo vidogo ambavyo havitaweza kumzamisha.

Kitu cha TANO tambuwa banda la vifaranga linatakiwa maranda ili kuongeza joto.

Kitu cha SITA tambuwa vifaranga vinatakiwa vifungiwe ndani kwa miezi miwili pekee.

Kitu cha SABA vifaranga havitakiwi kushikwa shikwa na mikono yako kila siku.

Kitu cha NANE vifaranga vinatakiwa kulishwa starter (nafaka nyembamba) na maziwa kwa kiasi.

Kitu cha TISA banda la vifaranga hutakiwi kulisafisha kila siku, hakikisha unasafisha mara tatu tu kwa wiki.

Kitu cha KUMI usije ukawapa chanjo wala dawa yoyote mpaka miezi miwili imalizike na banda lao linatakiwa liwe na majani...................

*UJUMBE usikate tamaa katika ufugaji mana hakunaga mwanzo mrahisi, changamoto ni mapito tu, jiamini mana hata wewe unaweza.*

1 Comments

Post a Comment

Previous Post Next Post