UFUGAJI WA KUKU WA KIENYEJI KAMA MTAJI.


MAHITAJI
Kuku(tetea) 10 na Jogoo 01
Banda bora
Vyombo vya chakula na maji
Chakula bora
Madawa na chanjo kwajili ya magonjwa
Chanzo cha nishati joto na mwanga
Elimu na ujuzi wa malezi bora
Chombo au chumba cha kutunzia vifaranga
Mayai ya kuku wa kisasa/mayai mabovu(ambayo hayakuanguliwa)
Madaftari au kitabu cha kutunzia kumbukumbu
KUKU 10

Wakati wa kuanza mradi wako hakikisha una kuku 10 (matetea) wenye umri sawa na hawajawai kutaga hata mara moja. Chagua kuku wenye rangi nzuri kutoka katika familia bora kutegemea malengo ya mradi wako. Mfano kama lengo lako ni kuzalisha kuku wa kienyeji kwajili ya nyama basi chagua mbegu ambayo inakuwa haraka na yenye uzito mkubwa. Au ikiwa lengo ni mayai basi ni vema kuchagua aina ya kuku yenye kukua haraka na kutaga mayai mengi.

Ili kupunguza gharama za manunuzi ya kuku na hivyo kuongeza faida kwa mfugaji ni vema kununua kuku wadogo ambao wametoka tu kuachishwa kulelewa na mama zao. Kuku hawa utawapata kwa bei ya chini, tena watafaa sana maana watakua na umri mmoja pia.

JOGOO 01
Jogoo mmoja tu anatosha kuwahudumia kuku matetea yote kumi. Hakikisha katika uchaguzi wa jogoo bora lililochangamka, rangi mzuri, upanga umesimama, macho angavu, uzito wa kutosha, rangi nzuri na uwezo mkubwa wa kuzalisha. Ni vema mfugaji akaelewa kwamba kuku wote watakaozalishwa watategemea ubora wa jogoo wake. Uwezo wa kutaga kwa kuku na upatikanaji wa mayai pia hutegemea kwa karibu ubora wa jogoo aliyechaguliwa.

BANDA BORA
Miongoni mwa mambo mhimu naya kwanza kuzingatiwa katika ufugaji wa kuku wa kienyeji kama mradi ni maandalizi ya banda bora. Kuku huhitaji banda bora ili wasiathirike na madhara mbalimbali. Mfugaji anatakiwa kuandaa banda lenye ukubwa wa mita 10 kwa mita 04. Yani urefu uwe mita 10 na upana upana wa mita 04. Kisha kata vyumba vya mita 2 urefu na upana mita 4 kutoka katika banda lako hivyo utakuwa na jumla ya vyumba vitano vyenye ukubwa unaolingana. Ujenzi uzingatie malighafi na vifaa vinavyopatikana kwa urahisi katika mazingira husika.

Mfano katika maeneo ambayo fitoKuku zinapatikana kwa urahisi banda linaweza kuandaliwa kwa miti na kukandikwa kwa udongo. Au sehemu ambayo mabanzi hupatikana kwa urahisi basi banda laweza kujengwa kwa kutumia mabanzi. Vifaa vya kujengea banda vizingatie pia gharama na upatikanaji wake katika eneo husika.

Baadhi ya vifaa hivyo ni kama ifuatavyo:-
Sakafu:
Saruji, udongo, mbao, mianzi au fito
Kuta:
Fito, mabanzi, mbao, nguzo mianzi,udongo, matofali, mawe, mabati na wavu
Paa:
Nyasi, makuti, majani ya migomba, mabati na vigae.
Wigo:
Matofali, mbao, fito nguzo, mabanzi, mianzi, matete, wavu na mabati.

Banda bora la kuku linatakiwa kuwa na sifa zifuatazo:-
Imara, lenye uwezo wa kuwahifadhi kiafya na pia dhidi ya hali ya hewa hatarishi kwa mfano jua kali, upepo, baridi na mvua pamoja na wanyama hatari.
Lenye mwanga, hewa na nafasi ya kutosha inayoruhusu usafi kufanyika kwa urahisi.
Lijengwe sehemu yenye mwinuko isiyotuama maji, isiyo na upepo mkali na iwe mbali kidogo na nyumba ya kuishi watu.
Liwe na vichanja kwa ajili ya kuku kupumzika na kulala.
Liwe na sehemu ya kuwekea chakula, maji, kutagia, kuatamia na sehemu ya kulelea vifaranga.
Liwe na nafasi ya kutosha kulingana na idadi ya kuku na kuweka vyombo vya chakula na maji.
Kwenye mazingira ya joto banda liwe la ukuta mfupi na sehemu kubwa wazi yenye wavu hadi kufikia kwenye paa. Kwenye mazingira ya baridi banda liwe na ukuta mrefu unaokaribia paa na sehemu ndogo tu iwe wazi yenye wavu ili kupitisha hewa na mwanga.

JINSI YA KUFANYA
Wakuze kuku wako hadi watakapofikia muda wa kutaga. Wakianza kutetea ni kiashiria kwamba wakati wa kutaga umekaribia hivyo andaa viota kwajili ya kutagia.

Viota vinapaswa viwe na ukubwa stahiki ili kumwezesha kuku kuyafunika mayai yote vizuri wakati wa kuetamia, viota viwe vinavyozuia mayai kutawanyika, viwe mahali pakavu na safi.

Hakikisha kuku wote wanataga katika viota tofauti. Kuku anapotaga mayai matatu unapashwa kuchukua mayai mawili na kumwachia yai moja ili kumfanya aendelee kutaga zaidi. Kuku akifikia yai la kumi na mbi

1 Comments

Post a Comment

Previous Post Next Post