MADAWA YA ASILI YA KUTIBU KUKU

Madawa ya asili ya kutibu magonjwa ya kuku ni mazuri kutumia kwa kuwa na faida zifuatazo;-

1.Hupatikana kwa urahisi. 2.Rahisi kutumia,
3. Gharama nafuu,
4. Zinatibu vizuri na HAZINA MADHARA.
Pia unaweza ukatengeneza unga wa mimea hiyo na kuchanganya kwenye pumba za Kuku.

SHUBIRI MWITU(Aloe vera).
 
Chukua majani 3-5 makubwa, katakata na loweka ndani ya maji lita 10 kwa masaa 12 hadi 16 Wape kuku kwa siku 5 - 7 Isiyotumika mwaga na tengeneza nyingine baada ya masaa 12 Mchanganyiko huu unaweza kutibu:
1. Kideri/Mdondo (Mdonde/Chikwemba/Kitoga/Chinoya/Sotoka) - inyweshwe kabla ya kinga. 
2. Homa ya matumbo (Typhoid).
3. Mafua (Coryza). 
4. Kipindupindu cha kuku (Fowl Cholera).

MLONGE
Mlonge una vitamin A na C. Chukua majani ujazo wa mikono miwili. Kisha yapondeponde na kuyaweka katika lita 10 za maji na iache kwa masaa 12-16, chuja na wape kuku. Isiyotumika mwaga na tengeneza nyingine. Mlonge hutibu:
1. Mafua.
2. Kideri - inyweshwe kabla kwa kukinga
3. Kipindupindu cha kuku (Fowl Cholera). 
4. Homa ya matumbo.

PILI PILI.
Ponda ponda, kisha changanya na maji na wawekee kuku wawe wanakunywa kwa muda wao. Inasemekana inasaidia kutibu mdondo (lakini mapema kabla maradhi kuingia). Dawa ya kutibu Kuku Kuharisha namna yoyote.

MPAPAI 
Kuandaa: Kata jani moja bichi la Mpapai na uliponde ponde lilainike kiasi. Kisha changanya na maji kiasi cha lita mbili na nusu. Kutumia (kwa tiba) - Kuku wapewe maji hayo wanywe,wasipewe maji mengine kwa ajili ya kunywa kwa siku angalau nne au zaidi, Inafaa zaidi kila siku kuwaandalia dawa mpya ili dawa isiharibike. Kutumia (kwa kinga) - Kupambana na magonjwa ya kuku

Jinsi ya kutibu na kuchanja - Hata kama kuku hawaharishi, wakizoeshwa kunywa maji yenye majani ya mpapai yaliyopondwa angalau mara tatu kwa wiki watakingwa magonjwa mengi. Njia nyingine ya kutumia Mpapai: Chukua majani ya Mpapai uyatwange upate kisamvu chake kiasi cha lita 1. Changanya kisamvu hicho na pumba 2kg. Waweza kuongezea maji kidogo na kuwapatia kuku wanaoumwa watumie chakula hicho hadi wapone. Kama kuku ni wachache, andaa chakula wa nacho kumaliza kwa siku moja ili kisibakie na kuharibika kabla hawajakimaliza.

By.....
#Dokta_Joh 
C.E.O #Ufugaji4Change
Call&WhatsApp 0764905449

9 Comments

  1. Daaaah nmeelimika vyakutosha asee mimi kama mfugaji ningependa uniadd kwenye group hilo iliniwe napata notification zakutosha💪🏿💪🏿🙏🏿🙏🏿

    ReplyDelete
  2. Nashukuru Sana kwa nimeelimika vya kutosha....

    ReplyDelete
  3. Asnte kwa elimu hii maana kuku wangu wanaumwa sana

    ReplyDelete
  4. Asnte Sanaa mungu akubaliki lakin vp pilipili haiwezi kutibu mafua

    ReplyDelete
  5. Nashukulu nimejua kiasigani anatakiwa Kula kifaranga na kwamuda gani mbarikiwe sana kwakutoa elimu hii

    ReplyDelete

Post a Comment

Previous Post Next Post