UFUGAJI WA SUNGURA

UTANGULIZI
Kabla hujaamua kufuga sungura hakikisha ya kwamba
umejitoa na una muda wa kuwahudumia wanyama waha,
ufugaji wao si rahisi kama vile ukifuga paka au mbwa, sungura
wanahitaji uangalizi na hassa kwenye usafi kwa sababu ni
rahisi kwao kupata maradhi yatokanayo na mazingira mabaya
na machafu
MABANDA
Kuna aina mbili za mabanda ya kufugia kwanza ni yale ya
kuwafungia ndani muda wote bila kutoka nje na ya pili ni ile
ya pili ni nusu nusu yaani wanakuwa na mabanda na
wanaweza kutoka nje kwenye ua maalum, katika aina zote
mbili ni muhimu kuhakikisha hakuna upenyo wa kuruhusu
panya kupita kwa sababu huwa wanakula watoto wa sungura.
UFUGAJI WA NDANI
1 – Usitumie banda la kioo (aquarium) kwa sababu halina
hewa ya kutosha na ni vigumu kusafisha
2 – Sakafu ya nyavu za waya ni nzuri zaidi ila hakikisha hakuna
sehemu zenye ncha kali inayoweza kuwaumiza sungura, kwani
wakumia ni mpaka wapone wenyewe au umchinje kwa sababu
ukitumia dawa za antibiotic sungura hana uwezo wa
kuzimeng’enya na kuisha mwilini mwake, siku ukimchinja
atabakia na dawa na hata ukinusa nyama yake utahisi harufu
ya dawa
3 – Ukubwa wa banda usipungue mita 4 * 2 kwa kila sungura
mmoja, likiwa kubwa zaidi ni vizuri
4 – Chini kuwekewe matandazio kama nyasi kavu au maranda
ya mbao, lakini maranda yatokanbayo na miti yenye mafuta
kama mi-pine na mikaratusi hayafai, wawekee kipande cha
blanket au taulo la zamani kwa ajili ya kulalia na kujifungulia
hasa kwa wazazi
5 – Ni muhimu kuwawekea sehemu ya kujificha mara
wanapohisi hatari, unaweza kutumia mbao, box gumu au
plastiki
UFUGAJI WA NJE
1 – Sehemu yote izungushiwe wavu wa kuku kuzuia panya
kuingia na wanyama wengine kama paka, mbwa, mwewe nk
2 – Upande mmoja uwe na mabanda, sehemu ya chakula na
maji pamoja na kivuli kwa ajili ya sungura kupumzika
3 – Futi moja chini ya udongo kuwe na zege kuzuia sungura
kuchimba na kwenda mbali
4 – Eneo la wazi liwe huru na hatari zote za sumu kama dawa
za kuulia wadudu au mbolea, pia majani yaliyoota yasiwe ni
yale yenye sumu (waone wataalamu wakushauri au ng’oa
yote)

Bonyeza link hii kutazama ufugaji wa sungura

https://youtu.be/CteP60P9C4M

MAJI
Tumia mabakuli ya kigae, plastiki au jengea kwa saruji, maji
yabadilishwe kila siku na vyombo visafishwe kila siku
CHAKULA
Wapewe majani, mabaki ya mboga za jikoni baada ya
kuchambuliwa, pia unaweza kuwawekea pumba au chakula
cha kuku (growers mash) kwenye vyombo maalum kama
chakula chenye virutubisho (concentrates)
USAFI
Kila siku jaribu kuondoa uchafu kama vyakula vilivyo mwagika,
na kinyesi kilichoganda kwenya matandazio, fagia na kubadili
matandazio angalau mara moja kwa wiki, manyoya ya sungura
mzazi yasiondolewe hii huonyesha kwamba anakaribia
kujifungua watoto
MENO
Wakati mwingine meno ya mbele hukua sana na
kumsababishia usumbufu wakati wa kula, waone wataalam
ukiona ni marefu zaidi na yanahitaji kupunguzwa, dalili kuu ni
sungura kushindwa kula kwa zaidi ya masaa 12
MIGUU
Miguu ya sungura si kama ya wanyama wengine, nyayo zake
zimefunikwa kwa manyoya, angalia ukiona yananyonyoka kuna
tatizo chunguza, kucha zake nazi huhitaji kupunguzwa zikikua
sana
UBEBAJI
Usimbebe kwa kutumia masiki yake huwa wanaumia sana,
shika ngozi nyuma ya shingo kama paka ukitaka kumbeba
DAWA
Wapewe dawa ya minyoo kama piperazine kila baada ya miezi
mitatu, dawa za wadudu kama akheri powdeer zinyunyuziwe
kwenya mabanda yao kuzuia viroboto, usiwape dawa nyingine
bila ushauri wa kitaalamu, antibiotics ndio usijaribu kabisa
kama nilivyosema mwanzo.

By Ufugaji4change
WhatsApp/Call. 0654237380

Post a Comment

Previous Post Next Post